TANGAZA BIASHARA SASA

Ijumaa, 29 Machi 2013

SHAA-LAVA LAVA VIDEO OFFICIAL


Mwanamuziki wa kundi la zamani la Wakilisha, Sarah Kaisi aka Shaa, ameachia video ya wimbo wake mpya, Lava Lava. Video hiyo imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab: Next Level. Akiongea na Bongofree hivi karibuni, Shaa alisema Lava Lava

GHOROFA LADONDOKA DAR

TAARIFA YA UHAKIKIKA KABISA ILIYOIFIKIA BF HIVI PUNDE INAELEZA KUWA JENGO MOJA LA GHOROFA 15 LILIPO JIRANI NA MSIKITI WA SHIA **ULIOPITA KATIKA MTAA WA IDRA GHAND,KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM,**LIMEPOROMOKA MUDA MFUPI ULIOPITA * * * *INAELEZWA KUWA MPAKA SASA WATU 17 WAMEOKOLEWA HUKU WAWILI WAKIWA WAMEPOTEZA MAISHA,NA JUHUDI ZA ZIADA ZINAENDELEA KUFANYWA ILI KUOKOA WENGINE WENGI WALIOFUKIWA NA KIFUSI HICHO.* * * *MKUU WA MKOA WA JIJI LA DAR ES SALAAM,MH. SAID MECK SADICK PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE MBALIMBALI WAPO ENEO LA TUKIO HIVI SASA AKISHIRIKIANA NA WADAU WENGINE

Ijumaa, 8 Machi 2013

SHAA KUACHIA VIDEO YA LAVALAVA KIMATAIFA ZAIDI

SHAA KUACHIA VIDEO YA LAVALAVA KIMATAIFA ZAIDI


Baada ya kuachia video ya wimbo wa Promise, Sarah Kaisi a.k.a Shaa haoneshi dalili za kupumzika mwaka huu, amedhamiria kusogea mbele zaidi kwa kuupeleka muziki wake kimataifa. Hivi karibuni alikuwa busy kufanya rehearsal na kushoot video ya ngoma yake mpya itwayo Lavalava inyoongozwa na Director mzoefu ndani ya bongo hapa si mwingine Adam Juma wa Visual Lab wa Next level.

   Akiongea na kwenye kipindi cha Exclusive friday ya Times FM leo..amesama anamalengo ya kuuvusha muziki wake kimataifa kwa mwaka huu na ndiyo maana ameshuuti video hii.
   Lengo langu ni kuangalia na kuvuka mipaka kwa hiyo video obvious nataka iende kimataifa lakini sina maana kuwa hapa mafans wangu hwataiona,Kwa wale wenye ving'amuzi,na wajanja wa kuperuzi kwenye internet wataiona tu 'alisema.

Jumapili, 3 Machi 2013

IRENY UWOYA AWEKA MAMBO YA NDANI HADHARANI ANGALIA


Huu  ni  upotofu  mkubwa  wa  maadili  unaoendekezwa  na  hawa  wanaojiita  MASTAA..... Kumbukumbu  zangu  zinaniambia  kuwa  Uwoya  ni  mzazi  wa  mtoto  mmoja  ambaye  walizaa  na Ndikumana  na hatimaya  wakaachana  baada  ya  kushindana  kitabia... Swali  la  kujiuliza  ni  kwamba, Anajisikiaje  kuyaanika  matako  yake  kwa  mtoto  wake  wa  kumzaa???...Atajenga  msingi  upi  kwa  mtoto  wake  akikua????..... Achilia ...

Cha  kushangaza ni kwamba  picha  hii  haimpi  shida   wala  aibu...... Yeye  anada  kwamba  "yuko  kikazi  zaidi".... Picha  hii aliipiga  wakati  wakirekodi  filamu  ya  ONE  BLOOD  ya  Tino  na  kuamua  kuisambaza.....  Hii  ni kali....Irene  Uwoya  kaamua  kutuzawadia  makalio  yake  na  shanga zake.....

MWANAMKE AFANYA MAPENZI MBELE YA MWANAE


Ni tukio  la  aibu   na  lenye  kuumiza  mno  lililotendeka  mbele  ya  mtoto  mdogo .Nimehuzunishwa na kuachwa na butwaa baada ya kuiona video ....Video hiyo sitaipachika hapa kwa sababu wanaosoma ukurasa huu ni watu wa umri na rika mbalimbali ambao Mpekuzi  haiwezi kuhakiki endapo kisheria wamevuka umri wa miaka 18 na wanaweza kutizama video hiyo. Huyu  ni  mama  wa  kizimbambwe  ambaye  alikuwa  akifanya  "mapenzi  ya  kuiba".. ..Hapa  namaanisha  alikuwa  "akisaliti"  na ndo  maana ...

Alhamisi, 28 Februari 2013

Audio track:Witney-Siko tayari[mke wa 20 percent

WEMA KUGEUKA LULU MTAANI

Ikiwa ni siku chache tu baada ya kufungua ofisi yake "endless fame", iliyoko maeneo ya mwananyamala, jana usiku wema alipokea simu akitahadharishwa na msamalia mwema kuhusu kundi la watu waliokuwa wanamzungumzia kwa kumpangia njama ya kumteka, watu ambao walikua katika moja ya baa ziliyoko Sinza ni jana tu around jioni.
''Wema'' nilipokea sim kutoka kwa msamaria mwema, akiniambia wema jihadhari, yaani baada tu ya kupokea hiyo sim, kwanza i was shoked halafu mwisho wa siku nikiona kama ma haters wanataka kunijaribisha, halafu mwisho wa siku kama vile hawawezi, maana hawajui how well am prepared......." wherever they are trying to do, they should just understand that, wasije wakajikuta wao ndio wako in trouble, in deep shit, because naskia kuna jopo la watu wanataka kunivamia and its not right, kama mwenzako anafanikiwa muombee mema sio kumdidimiza...."amesema Wema source na gumzo la jiji

MASIKINI LADY JAYDE AOMBA MSAADA MTANDAONI

MASIKINI LADY JAYDE AOMBA MSAADA MTANDAONI


-- 
Mwanamuziki wa muda mrefu, Lady JayDee a.k.a Binti Komando yuko mbioni kuachia wimbo wake mwingine mpya kabisa utakaokwenda kwa jina la ''JOTO, HASIRA''.

Jaydee amekuwa kimya kidogo kwenye kuachia ngoma mpya kwa muda mrefu sasa, na sasa anarudi tena na ngoma hiyo ambapo ndani yake amemshirikisha rapper wa muda mrefu pia,Profesa Jay.

Jide mapema masaa machache yaliyopita, alitupia CD covers tofauti za wimbo huo kupitia ukurasa wake wa Facebook huku akiomba ushauri kwa mashabiki wake kuweza kumchagulia MOJAambayo itaweza kutumika kwa ajili ya wimbo huo.
Check covers zenyewe hapa chini:

Audio track:TID ft PROFESA J - RAHA

Audio track:Aloneym-Olewa

Audio track:Man Walter-Nawaogopa

SOGGY DOGGY ATIMKIA IRINGA RASMI

Msanii/Mtangazaji Soggy Doggy ameacha mzigo pande za redio Uhuru na leo rasmi ameondoka Dar es salaam nakwenda Iringa ambapo atakuwa akifanya kazi katika kituo kingine cha Redio kinachoenda kwa jina la Ebony Fm.Soggy Doggy ashawahi kufanya kazi katika vituo vya redio mbalimbali hapa nchini kama Arusha na Mwanza.

LINEX AMVISHA PETE YA UCHUMBA MPENZI WAKE

Weekend hii, mtu mzima Sunday Mjeda aka Linex aka Mr VOA (Voice Of Africa),
 alifanya yake kwa 
kumvisha pete mpenzi wake, ambae ni  ambae ni  mwenyeji wa Finland anaeitwa Suvi.
  Linex aliamua kufanya 
kimya kimya tena wakiwa wawili tu,
 kwasababu hakutaka kujionyesha, na anaamini ile ni kitu
very personal haikuhitaji manjonjo mengi...all in all This is Diamond hii
inakutakia kila la kheri...!!


MWANA FA :MSANII MWENYE VIPAJI LUKUKI
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' aeleza, kuwa na kipaji zaidi ya kimoja ndio sababu ya kipekee inayomtofautisha yeye pamoja na kazi zake na baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa bongofleva
Aliyazungumza hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati yake aliyokuwa nayo ya kuiachia nyimbo yake mpya hivi karibuni inayoitwa 'Kama Zamani'ambapo mashabiki wake watapata fursa ya kuisikia nyimbo hiyo katika vituo vya redio mbalimbali nchini, alisema kipaji ndicho kinachompa fursa ya kufanya muziki katika ngazi ya kimataifa

Alisema muziki unamatawi mbalimbali kwani kuna baadhi ya wasanii wanakipaji cha kuimba tu lakini hawezi kufanya shoo katika 'stage' wapo baadhi wanajua kuandika na hawajui kuimba wapo wengine wanajua kufanya vyote kwa wakati mmoja

Akizungumzia kwa upande wake Mwana Fa alisema amejaaliwa kuwa na vipaji vyote kwa wakati mmoja huku akiwa na uwezo wa kuandika mashairi, kuimba pamoja na kulimiliki jukwaa pindi awapo katika shoo

"Nimejaliwa vipaji vyote hivyo, kwani nina uwezo wa kuandika mistari mizuri, kuimba na kulimiliki jukwaa na ndio maana shoo zangu zinakuwa na mvuto wa kipekee kutokana, sanaa na ubunifu niliokuwa nao " alisema Mwana Fa

Akizungumzia ujio wa wimbo wa 'Kama zamani' wenye mahadhi ya Hip Hop ambapo msanii huyo amewashirikisha baadhi ya wasanii kama Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje), alisema kuwa ameamua kushirikisha wasanii hao ili kuleta radha tofauti ya muziki na mashabiki wapate muziki ulio bora
Alisema kuwa nyimbo hiyo italeta mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki kulingana na ubora uliopo, kwani imetengenezwa 'live' kinanda, gitaa vyote vinasikika kwenye muziki huo, chini ya mtayarishaji Pfunk Majani

EMA THE BOY:MWALIMU ALIEIBUKIA UTENGENEZAJI WA MUZIKI BONGO

KUJITUMA ni msingi wa mafanikio na kuthamini kile ulichonacho kama unavipaji zaidi ya kimoja jiwekee mikakati thabiti ya kuweza kuvitumia vyote kwa pamoja ili kuweza kufanikisha malengo yako uliojiwekea hayo ni maneno ambayo anayatumia prodyuza wa Surround Sound studio Emanuel Maungu anajulikana kwa jina la Ema Theboy katika msingi wa kuyaongoza maisha yake alipokutana na Spoti Majira wiki hii

Mbali na kutengeneza muziki taaluma yake ni mwalimu, ambapo alianza mafunzo hayo ya ualimu mwaka 2010-2012 daraja la tatu A huku akiwa amepangiwa mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kufundisha,ingawa kwa kipindi hicho chote anafanya kazi ya kutengeneza muziki

Baada ya kumaliza masomo yake ya O level ndipo alipopata nafasi ya kujiunga na chuo cha ualimu mkoani Tanga, ambapo aliweza kufanikiwa kusoma kwa kipindi cha miaka mitatu, na kuweza kuhudhuria masomo kwa vitendo na kukumbwa na changamoto kadhaa kama mwalimu, huku akiweka wazi kuwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika ni moja ya changamoto kubwa wanayokutana nayo wawapo katika mazingira ya kazi hiyo

Alianza kupenda muziki tangu akiwa mwanafunzi ambapo alijiunga na kwaya kanisani ili aweze kupata nafasi ya kujifunza kutumia baadhi ya vyombo vya muziki ikiwemo Kinanda, ingawa aliweza kufundishwa 'key' moja ya herufi A, kutokana na juhudi zake binafsi aliweze kumudu kujifunza key nyingine ambapo mpaka sasa ndio muongozo wa kazi zake

Kutokana na hali ya kupenda kutengeneza muziki alijikuta akilazimika kujiunga na Nyumba ya kukuza Vipaji (THT) mwaka 2012 ambapo alianza kujifunza kutumia 'Technology' mpya ya  kuhamisha muziki kwenye kinanda na kutumia computa kutengeneza muziki

Kutokana na ugumu wa technology alikaa wiki moja  bila ya kuingia studio ili aweze kujipanga na kujifunza huku akipata darasa la walimu kuhusu matumizi ya technoilogy hizo mpya ambazo kwake zilikuwa ngeni

Hali hiyo iliweza kumsaidia na kumudu kutengeneza muziki i wenye hadhi ya kimataifa na kujitofautisha na maprodyuza wanaofanya muziki wa kuchora

Kazi yake ya kwanza kama Prodyuza ilikuwa ni kutengeneza nyimbo ya 'Upepo' iliyoimbwa na msanii Recho wa kutoka kundi la THT alichukua wiki nzima kuikamilisha wimbo huyo huku akiwa amesimamiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kupata muongozo na kuboresha nyimbo hiyo

Kwa kuwa ni nyimbo yake ya kwanza na alikuwa anaamini kile anachokifanya, hivyo aliamini kuwa nyimbo hiyo ingeweza kufanya vizuri na ndivyo ilivyokuwa kwani nyimbo hiyo ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri katika 'gemu' la muziki nchini

Prodyuza huyo hakuishia hapo aliamua kujiwekea mikakati iliyothabiti ili aweze kuboresha kazi zake kwani ameweza kuendelea kutengeneza muziki wenye radha tofauti huku akiamini kuwa hawezi kusikiliza muziki alioutengeneza kila wakati ili kuepusha kurudia rudia nyimbo zinazofanana

"Napenda kuwa mbunifu kwenye kazi zangu naepuka sana kurudia kazi hivyo nina mikakati iliyo thabiti ili kuendelea kuboresha kazi zangu ziweze kuwa nzuri n zenye kuvutia"

Ili kuonyesha kuwa anaendelea kuifuata mikakati yake ya kutengeneza muziki yenye ubora na kujitofautisha na maprodyuza wengine ameweza kutengeneza nyimbo nyingine zinazofanya vizuri kwenye 'gemu' la muziki 'Me and U' ya msanii Ommy Dimpoz, pamoja na nyimbo ya Barnaba inayojulikana kwa jina la 'Sorry'

Siku za mapumziko anapenda kuangalia katuni na movi, huku rangi anayoipenda zaidi ni blue na nyeusi

Ameweka wazi kuwa anamchumba anayempenda huku akisisitiza mwanamke anayempenda ni yule anayeelewa kitu anachofanya na kuthamini pamoja na kuheshimu yake anayoyafanya

DOGO JANJA AONJA NDEGE KWA MARA YA KWANZA


Dongo janja ambae kwa sasa yuko chini ya usimamizi wa Mtanashati Entertainment na Ostz Juma na musoma, ameshadondoka nchini Africa ya kusini kwa ajili ya kuanza kazi moja tu ambayo imempeleka huko, ikiwa ni makamuzi kwa kwenda mbele, na akisisitiza kuwa show yake ya kwanza itafanyika ndani ya cape town.
janjaro anaonekana kwenye picha kupokelewa vizuri na mashabiki wake na watanzania waliopo huko, na baada ya kufumbua macho kwa mara ya kwanza na kuyasafisha kwa majengo mazuri na hali ya hewa tofauti na home, aliamua kuwapa moyo vijana wenzake  kupitia ukurasa wake wa facebook,wanaofanya mziki kwa kuwashauri wasikate tamaa..

Thnx God nlifika South Africa salama Now nipo Cape town ambako show yangu ya kwanza itafanyika ndani ya jiji la cape town... Nawapenda mashabiki wangu.... Kama upo cape town au south africa... Kaaa mkao wa kula... Nawapenda watanzania wooote na watu wooote... Nipo na Ostaz Juma bigBoss .. So, nipo na Boss wangu.. Naenjoy sana huku najifunza vitu vyingi pia ndio mara ya kwanza kudondoka wanangu ambao bdo hamjatoboa kimziki kazeni.. Mi sikati tamaa na sitoridhika nataka niende mbali zaidi ya hapa...nataka niende mbaliii saaalute sana kama ww ni shabiki wa Janjaro na unapenda maendeleo yangu Comment au like.... Pamoja..

RICK ROSS:RAPPER ANAEISHI KWA MASHAKA MAREKANI

Rick Ross, rapper ambaye amekuwa akilengwa kushambuliwa na kundi la wahuni, ameongezewa ulinzi na polisi wa jijini New York, Marekani…. saa 24 kwasababu ya kupokea vitisho vingine. Kwa mujibu  wa mtandao wa TMZ, polisi wamekuwa wakimlinda Ross aliyefikia kwenye hoteli ya the London .
Vyanzo hivyo vya habari vimeuambia mtandao huo kuwa rozay ajachukulia matukio hayo kawaida ndiyo maana amepewa ulinzi mwezi uliopita alinusulika kupigwa risasi alipokuwa anendesha bgari lake aina ya rolls-royce huko Ft lauderdale muda mfupi baada ya kutoka kwenye party yake ya kuzaliwa.

Jumapili, 24 Februari 2013

P FUNK MAJANI;PRODUZA MWENYE REKODI KUBWA GEMU LA MUZIKI BONGO

KUTOKANA na kuwa na upungufu wa maprodyuza kwa miaka ya 1990 hali ilisababisha kunishawishi kuwa prodyuza ili kuutambulisha muziki wa Tanzania katika mataifa mbalimbali nje ya fani ya kutengeneza muziki, ni muimbaji mzuri hususani wa Hip Hop hayo ni maneno yaliyokuwa yanazungumzwa na prodyuza Paul Matthysse anayejulikana kwa jina la P Funk Majani alipokutana na Spoti Majira wikii hii

Alianza kupenda kufanya muziki mwaka 1992 huku akiwa ameunda kikundi cha muziki kilichokuwa kinajulikana kwa jina la 'Street Wisdom' kwa kipindi hiko alitumia muda wake mwingi kufanya muziki kwani ndio kitu alichokuwa akikipenda

Alikuwa anapenda kuimba muziki wa Hip Hop kwa kipindi hiko cha miaka ya 90, ingawa kwa sasa ni produza anamiliki studio ya Bongo Records, huku akibainisha kuwa studio hiyo imewatoa mastaa wengi akiwemo msanii Juma Nature na wengine wengi

Kutokana na hali ya kupenda kufanya Hip Hop alijikuta analazimika kubadili fani na kuingia katika prodyuza huku akiwa na ndoto lukuki za kutengeneza muziki wenye ubora wa kimataifa na kuutangaza muziki kwenye ngazi ya kimataifa

Kwa kipindi chote hicho aliweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa kuutambulisha muziki hapa nyumbani na kuleta changamoto tofauti hali iliyosababisha mapokeo ya muziki huo kuwa mazuri na mashabiki kuukubali muziki wa bongo fleva

Alianza safari ya kuwa produza mwaka 1997 wakati ambao watu wengi hawaelewi muziki na kulikuwa na dhana tofauti tofauti huku baadhi ya watu wakidai anayefanya muziki ni muhuni wengine wakidai muziki ni wa watu furani kwenye jamii

Aliweza kung'araa zaidi alipokuwa Produza kwa kukuza vipaji vya wasanii wengi na kuufanya muziki wa Tanzania uweze kujulikana ndani na nje ya nchi huku akibainisha kwamba albamu ya Feruz Mrisho iliyobeba jina la Starehe ndiyo iliyoongoza kwa mauzo kwa kufikia nakala 500,000 katika wasanii wote waliokuwa kwenye lebo yake

Hakuwa nyuma kwa kuwa na mikakati ya kuufanya muziki utambulike kwani alikuwa ni mtu ambaye anaweza kuandaa 'concert' za uzinduzi wa albamu mbalimbali za wasanii waliokuwa chini ya lebo yake na aliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani mpaka sasa hakuna msanii aliyeweza kuipita rekodi ya Juma Nature wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya Ugali alipoweza kujaza mashabiki katika ukumbi wa Diamond

Mikakati hiyo bado anaendelea nayo kwa kuwaomba wadau wa muziki wajitokeze kudhamini shoo hizo kwani wananchi na mashabiki bado wanahitaji kuona wasanii wao wanafanya uzinduzi wa aina hiyo, hali hiyo itasababisha kuepusha  wasanii kufanya uzinduzi wa single zao katika club huku idadi ya mashabiki wakizidi kupungua siku hadi siku

Kwa sababu ya kupenda kuimba muziki wa Hip Hop mwaka jana prodyuza Pfunk aliamua kufufua kundi la muziki linaloundwa na watayarishaji wakali wa muziki wa bongo fleva akiwemo John Mahundi, Lamar huku wakiwa wameachia single yao inayojulikana kwa jina la 'No Name'

Siku za mapumziko anapenda kwenda ufukweni kupunga upepo huku akiamini kuwa mawazo mapya na ubunifu mwingine anaupata akiwa katika maeneo hayo ya ufukwe

Anapenda sana rangi nyekundi na huchagua rangi nyekundi kwenye mavazi yake huku akiamini kuwa rangi hiyo humaanisha hatari ingawa si hatari kwenye maisha yeake

JINA LA WIMBO LAMKIMBIZA STUDIO; PHILPO

Msanii chipukizi wa miondoko ya Hip hop&Rnb nchini Tanzania Philpo maarufu kama King of Airport ameitonya safu hii kuwa yupo mbioni kuachia wimbo wake mpya,ambao bado ajaupatia jina rasmi.

 Akiongea na mwandishi wa Bf kwa njia ya simu kutoka wilayani Tunduru ambako ndiyo makazi yake amesema yupo studio kwa ajili ya maandalizi ya ujio wake wa pili baada ya kutamba na wimbo wake wa Special 4 mother.Amewaomba mashabiki kumpokea tena na kazi hiyo ambayo ana amini itampeleka level zingine.

   Alisema'kiukweli huu wimbo utafanya mapinduzi makubwa kwenye gemu la hip hop,ukizingatia kuwa upo katika maandalizi ambayo ni ya kisasa zaidi na unaendana kabisa na gemu jinsi linavyokwenda kwa sasa.Pia naomba menejiment ya kunisimamia kwa sasa kwani nashindwa kujimeneji kwa sababu nakosa maneja...kama atatokea meneja tuwasiliane kupitia hii namba yangu 0788269853.
    
Msanii huyo pia alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa muziki bado mikoani hupo kwa kiwango kikubwa isipokuwa wamekuwa wakishindwa kupata sapoti ya kuwapeleka mbele kutokana  na muamko mdogo wa wadau...kwani Dar itabaki kuwa soko kuu la muziki tu na si vipaji vilivyopo mikoani alisema

HATIMAE MRITHI WA SHARO APATIKANA

SHAROMILIONEA
MRITHIHATIMAYE ametokea mrithi wa marehemu Sharomilionea ambaye anaimba muziki na kuigiza miondoko yote iliyokuwa ikifanya na marehemu huku akiwa ameongeza vionjo vingine ili kuweza kuwateka mashabiki wake

Mrithi huyo anayejulikana kwa jina la Ramadhani Mohamed ambapo jina la kisanii anajulikana Sharomaburudani, akizungumza na Spoti Majira alisema kuwa kutokana na kufanana na marehemu Sharomilionea baadhi ya watu walimshauri kufanya kazi ambazo zilikuwa zinafanywa na marehemu

Alisema kuwa mbali na kufanana kwa miondoko ya kutembea na swaga pia anafanya muziki na sanaa ya vichekesho kwa kutumia mitindo ya marehemu ingawa amejalibu kuwa mbunifu kwa kuongeza vionjo vidogo mwishoni ambavyo vitaongeza radha zaidi

"Mimi nafanya kila kitu kama yeye ingawa nimejaribu kuongeza vitu vingine vyenye swaga za tofauti tofauti na ninatumia zaidi swaga za 'Black America'kuanzia mavazi hadi kuongea " alisema Sharomaburudani

Aliongezea kuwa ili kuthibitisha kuwa anauwezo wa kumrithi marehemu Sharomilionea hivi karibuni atatoa single yake inayokwenda kwa jina la 'darasa' ambayo imefanywa chini ya studio ya Wajukuu iliyopo Mbagara jijini Dar es Salaam

Alitoa wito kwa wadau na mashabiki wa sanaa kiujumla hususani muziki kutoa ushirikiano kwenye sekta hiyo ili kufikisha muziki wa bongo fleva katika hadhi ya kimataifa

Jumatatu, 18 Februari 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 HAYA HAPA


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
Idadi ya Wavulana
Idadi ya Wasichana
Jumla
I
1,073
568
1,641
II
4,456
1,997
6,453
III
10,813
4,613
15,426
I-III
16,342
7,178
23,520
IV
64,344
38,983
103,327
0
120,664
120,239
240,9036.0        SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average”(GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5.  Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule yakwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :

NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
ST. FRANCIS GIRLS
90
MBEYA
2
MARIAN BOYS S.S
75
PWANI
3
FEZA BOYS S.S
69
DAR ES SALAAM
4
MARIAN GIRLS S.S
88
PWANI
5
ROSMINI  S S
78
TANGA
6
CANOSSA S.S
66
DAR ES SALAAM
7
JUDE MOSHONO S S
51
ARUSHA
8
ST. MARY’S  MAZINDE JUU
83
TANGA
9
ANWARITE GIRLS S S
49
KILIMANJARO
10
KIFUNGILO  GIRLS S S
86
TANGA
11
FEZA GIRLS
49
DAR ES SALAAM
12
KANDOTO SAYANSI GIRLS SS
124
KILIMANJARO
13
DON BOSCO SEMINARY SS
43
IRINGA
14
ST.JOSEPH MILLENIUM
133
DAR ES SALAAM
15
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS
64
KIGOMA
16
ST.JAMES SEMINARY SS
44
KILIMANJARO
17
MZUMBE SS
104
MOROGORO
18
KIBAHA SS
108
PWANI
19
NYEGEZI SEMINARY SS
68
MWANZA
20
TENGERU BOYS SS
76
ARUSHA7.0        SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

NAFASI
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
MIBUYUNI S.S
40
 LINDI
2
NDAME  S.S
41
UNGUJA
3
MAMNDIMKONGO S.S
63
PWANI
4
CHITEKETE S.S
57
MTWARA
5
MAENDELEO S.S
103
DAR ES SALAAM
6
KWAMNDOLWA S.S
89
TANGA
7
UNGULU S.S
62
MOROGORO
8
KIKALE S.S
60
PWANI
9
NKUMBA S.S
152
TANGA
10
TONGONI S.S
56
TANGA

9.0           MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWABaraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:

(a)           Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miakamiwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.

(b)           Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.10.0        MATOKEO YA MITIHANI  YALIYOFUTWA


S/N
AINA YA UDANGANYIFU
IDADI YA WATAHINIWA
(i)        
Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.
04
(ii)       
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’
170
(iii)      
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.
590
(iv)      
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.
04
(v)       
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.
06
(vi)      
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.
15

JUMLA
789


Distributed ByMy Blogger Themes|Designed ByBloggerMotion

Top - See more at: http://chimachibueze.blogspot.com/2014/07/how-to-create-facebook-comments-box-on.html#sthash.VQrs8WAL.dpuf